jamaa wawili wako baa wakipiga gambe na stori.wakwanza akasema hivi ulisikia mike alikufa?
wa pili;hapana.ilikuwaje kwani?
wa kwanza:alikuwa anakuja nyumbani kwangu akiendesha gari yake. sasa alikuwa spidi kali na hakushika breki vizuri kwahio gari yake ikagonga geti na kubilingita na yeye akarushwa mpaka ghorofa yangu ya kwanza na akapasua kioo akadondoka chumban.
wa pili,'dah,kifo kibaya sana.
wa kwanza,hakufa,baada ya kugaagaa akaona kabati la nguo na akashika mshikio wake ili ajivute asimame ila kabati lote likamdondokea na kumvunja mifupa yake mingi tu.
wa pili;maskin, kifo kibaya
wa kwanza,'hakufa bado.alitambaa mpaka akatoka chini ya kabati hadi nje ya chumba.akashika ukingo wa ngazi zilizokuwa zinashuka chini.sababu ya uzito wake na jinsi alivyokuwa amezishika hizo kingo zikavunjika na yeye akaanguka hadi chini na kingo zikamponda kwa juu.
wa pili huku akitikisa kichwa,'mama yangu.kifo gani kibaya ivo....'
wa kwanza;aliweza kupona hilo.akatambaa mpaka jikoni akataka ajivute asimame bahat mbaya akashika mkono wa sufuria lililokuwa na maji ya moto.yote yakamwagikia na kumbandua ngozi ya sehm kubwa tu.
wa pili,'hicho kifo kinasikitisha sana
wa kwanza hakufa;alijikaza akaona simu akataka apige watu wamsaidie lakin akashika waya wa umeme badala ya wa simu na alipouvuta ukakatika.umeme na maji havipatani, akapigwa shoti kubwa sana.
wa pili;mama weee.hicho kifo kinatia huruma sa...
wa kwanza;hakufa hapo ali.....
wa pili;sasa niambie alikufaje....
wa kwanza;nlimpiga risasi
wa pili;kisa?
wa kwanza;ALikuWa ANa haRiBu NyumbA Yangu.............
No comments:
Post a Comment