Wednesday, September 19, 2012

Mke. wa kamikaze alikuwa anafuga paka na jason alikuwa anamchukia sana yule paka. Siku moja akaamua kwenda mtupa mbali, akamchukua na gari kilomita 1, akamuacha paka hapo kurudi home. Alipokua anakaribia kwake akamuona paka naye anaingia ndani.. akashangaa kweli..akauchuna.
Siku iliyofuata akamchukua paka na kumpeleka mbali zaidi kilomita 5 kutoka nyumani kwake.. akumtupa hapo na kurudi nyumbani.... alipokaribia nyumbani kwake akamuona tena paka naye amerudi anaingia ndani... akasema moyoni kesho utanitambua!!
kesho yake akaamka na kumchukua paka akaenda mbali zaidi kilomita 50 akakata kushoto akakata kulia akanyoosha tena kushoto kulia akazunguka saaaana!... kisha akamtupa paka, akaanza safari ya kurudi home... baada ya muda akapiga simu kwa mke wake nyumbani.
Jamaa: "Mke wangu vipi.... huyo paka yupo apo?"
Mke: "Ndio mume wangu yupo katulia tu, vipi imekuaje?"
Jamaa: "Hebu mpe simu anielekeze njia ya kurudi nyumbani... maana mi nimepotea."

No comments:

Post a Comment