Friday, August 3, 2012

VITUKO USWAHILINI

VITUKO USWAHILINI
Jamaa flani kaingia kinyozi,wakati yuanyolewa kukaingia dem msupa.Jamaa akaamua kujaribu bahati yake.

JAMAA:"Mambo?"
MSUPA:"Poa"

JAMAA:"Mi na wewe tunaeza meet baadae?"
MSUPA:"Kwanini?"

JAMAA:"Kwa sababu umenibamba nataka nikupeleke date"
MSUPA:"Sawa,lakini nitamwambia nini mume wangu?"

JAMAA:"Aaah...hilo si tatizo mdanganye tu! Mwambie umeenda kutembelea rafiki yako hospitalini"
MSUPA:"Mwambie mwenyewe....huyo hapo anakunyoa!"

JAMAA:"Duh..!"

No comments:

Post a Comment