Wednesday, September 19, 2012

Translator wuuuuh

Jamaa flani baada ya kuchoma
bangi zake,akatoka na kuenda
kuingia duka la muuza nyama.
Mara kukaingia paka,akaanza
kulia....Miaaao w! Miaaaow!
Jamaa akamwambia muuza
nyama,"Huyu paka anataka robo
kilo ya maini."
Paka akapewa,akaila yote kisha
akaanza tena kulia,Miaaaow!
Miaaaow..miaaow !
Jamaa akamwambia muuza
nyama tena,"Sasa anataka robo
kilo ya nyama.
Paka akapewa akaila yote,kisha
akatoka akaenda zake.
Mwenye duka akamwambia
mvuta bangi,"Haya lipa robo kilo
ya maini na robo kilo ya nyama."
Mvuta bangi akajibu,"Mie
yananihusu nini? Nilikuwa na
TRANSLATE tu!!"

No comments:

Post a Comment