Thursday, June 21, 2012

LAUGH! LAUGH! TILL WE DIE!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!

WATOTO WENGINE PRESHA TUPU
Baba na mama,ni matumaini yangu kuwa mtasoma
ujumbe wangu huu kwenye karatasi niliyoiweka
juu ya meza,naomba msishtuke mana ni mambo ya
kawaida kwenye maisha tunayoishi,najua
mtaumia kwa vile bado nasoma
na ndo nipo kidato cha kwanza,Napenda kuwajulisha kwamba sasa hivi mnaposoma hii
barua sipo nyumbani,nimetoroka mana
nimegundua nina uwezo wa kujitegemea kwa
sababu mi ni kijana mwenyewe umri wa miaka 14
na ninajua kipi chema na kipi kibaya.tangu mwezi
mmoja uliopita nilikuwa na uhusiano na binti mmoja aliyeitwa Rachel,mwenye umri wa miaka
27 na kwa sasa ndo naishi naye kwenye chumba
alichopanga.Nilipokuwa nyumbani sikuwa napata
hela za kutosha ila sasa nimeanza kushika noti za
shilingi 10,000,msichana niliyenaye ni mzuri sana
wa umbo na ninampenda sana,amenifundisha njia za kutafuta hela.Amenipangia kazi ya kuuza
madawa ya kulevya na yeye ikifika usiku anaenda
kuuza mwili wake,basi kila siku tunapata hela ya
kutosha,huyu mchumba wangu ni msichana
mwenye bidii,kwa siku analala masaa 6 tu maana
mwanaume yeyote akija lazima awe naye chumbani kwa mda wa masaa 3.Msiwe na
hofu,nipo salama kabisa na nimeamua kumwoa
Rachel mana ni kila kitu kwangu.
Pia amenunua gari la kubebea mbao kwahiyo
biashara inaenda vizuri,Rachel ameenda kupima
afya na amekutwa na upungufu wa kinga mwilini,mara
nyingi namridhisha anapotaka kitu flani,iwe
kufanya naye mazoezi ya viungo au kufanya naye
mapenzi,si mnajua unapokuwa na mgonjwa
unakuwa naye karibu,ila mi pia sijihisi vizuri mana
kila saa nakohoa tu na sina uhakika kama nimeathirika,.Tumepanga baada ya miaka miwili
tutawatembelea,nadhani mpaka miaka miwili iishe
atakuwa ameshajifungua,na nifuraha yangu
mtamwona mjukuu wenu.Wazazi wangu sina la
kuongeza kwaherini Mungu akipenda tutaonana.
Baba na mama mi nipo chumbani kwangu, mnachokisoma ni h/work ya mwalimu wa
kiswahili alituambia tutunge hadithi fupi,naomba
iangalieni kama kuna makosa ---------
Nadhani mama asingemalizia hii yani siku mingi
keshazimia.

No comments:

Post a Comment